FADAK YA SAYYIDAT FATIMA (S.A). KUHUSU HOTUBA YA SAYYIDAT FATIMA (S.A) NDANI YA MSIKITI WA MTUME (S.A.W.W) IKIHUSIANA NA KADHIA YA FADAK. Sehemu ya 21

Mwenyeezi Mungu (s.w) ameifanya “IMANI” kuwa ni kitu kitakacho watwaharisha wanaadamu kutokana na shirki ya kumshirikisha.Na akaifanya “SWALA” kuwa ni kitu kitakacho watakasa kutokana na kibri.Kisha akaifanya “ZAKA” kuwa ndio kitu kitakacho zitakasa nafsi

Mwenyeezi Mungu (s.w) ameifanya “IMANI” kuwa ni kitu kitakacho watwaharisha wanaadamu kutokana na shirki ya kumshirikisha.Na akaifanya “SWALA” kuwa ni kitu kitakacho watakasa kutokana na kibri.Kisha akaifanya “ZAKA” kuwa ndio kitu kitakacho zitakasa nafsi za wanaadamu, na kuzidisha riziki zao.Na akaifanya “SWAUMU” kuwa ni kitu kitakachoimarisha Ikhlasu (yaani kutenda kwa nia safi,kwa nia iliyotakasika,kwa ajili ya Allah -s.w-).Na akaifanya HIJJA kuwa ni kitu kitakacho Imarisha dini Tukufu ya Kiislam.Na akaufanya “UADILIFU” kuwa ni kitu kitakachoweka nidhamu au mpangilio uliokuwa mzuri katika nyoyo za wanaadamu ili kuziponesha nyoyo hizo za wanaadamu

Add new comment